Jeshi la Polisi Mkoani Iringa limefanikiwa kumkamata Mtuhumiwa na Mfanyabiashara Kaloli Mkusa mwenye umri wa miaka 30 ambaye alihukumiwa kwenda Jela miaka 30 na fidia ya shilingi million moja kwa kosa la kumbaka mama yake Mzazi katika kijiji cha kisisina.
Mkusa ambaye alikuwa akifanya biashara Tunduma mkoani Songwe alihukumiwa wiki moja iliyopita huku akiwa ametoweka kusikojulikana kutokana yeye pamoja na baba yake mzazi Joseph Mkusa ambaye alimuwekea Dhamana.