Aliyekuwa mgombea wa urais wa Shirikisho la Soka Tanzania, Ally Mayay, amekiri kuwa amestahili kukatwa katika kinyang’anyiro hicho kutokana na kutofikisha idadi ya wadhamini watano walitakiwa.
Mayay na mwanahabari Osca Osca ni kati ya wagombea walioenguliwa na Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa madai ya kushindwa kukidhi vigezo vya kikanuni.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam, Mayay amefafanua kuwa aliwasilisha vitu vyote vinavyotakiwa ikiwamo vyeti lakini upande wa wadhamini hawakukamilika.
“Kati ya vitu vilivyotakiwa kuwasilishwa kwenye kama ni kitambulisho cha uraia, vyeti vya shule na barua za wadhamini watano, lakini mimi nimepata mdhamini mmoja,” Mayay.
Ameeleza kuwa amejitahidi kuomba udhamini katika klabu zote 18 za Ligi Kuu Tanzania Bara ila mmoja ndiye alimuunga mkono.
“Nitaendelea kutoa mchango katika soka kwa nafasi nilikuwa nayo, pia nipo tayari kutoa ushauri kwa wagombea wakihitaji sera zangu nilizotakiwa kuwasilisha kipindi cha kampeni,” Mayay