Headlines za wachezaji wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa Dunia kwa mwaka 2015 (Ballon d’Or) bado zinazidi kuchukua nafasi, kwa sasa kila mmoja amekuwa akitaja mshindi wake katika tuzo za Ballon d’Or 2015, baada ya November 30 kutangazwa majina matatu yaliofanikiwa kuingia fainali ya tuzo hizo zitakazotolewa Zurich Uswiss January 11 2016.
Baada ya mashabiki wengi wa soka kuongea au kutaja kila mchezaji wake anayedhania kuwa anastahili kuwa mshindi wa tuzo ya Ballon d’Or kati ya Lionel Messi, Neymar na Cristiano Ronaldo, December 4 imekuwa ni siku ya beki wa klabu ya FC Barcelona ya Hispania na timu ya taifa ya Brazil Daniel Alves kuzungumza au kutaja mtu anayestahili kushinda tuzo hiyo.
Alves hakuishia kumtaji Lionel Messi pekee kuwa ndio atakuwa mshindi January 11 2016 kati ya majina ya wachezaji hao watatu waliofanikiwa kuingia katika kuwania tuzo hiyo, bali amesema Cristiano Ronaldo hakustahili kuwa nominated katika Top 3 hiyo, kwani mchezaji bora wa Dunia sio kufunga magoli pekee.
“Messi atashinda kutokana na mchango au ushawishi wake katika mchezo, nafikiria Neymar kwa sasa ndio wa pili kwa ubora baada ya Lionel Messi , Cristiano Ronaldo hakustahili kuwa katika tatu bora ya wanaowani tuzo ya Ballon d’Or kwani hii haiusishi ufungaji pekee” >>> Daniel Alves
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.