Shirikisho la soka Tanzania TFF leo Septemba 13 2016 limetangaza rasmi kupitia afisa habari wake Alfred Lucas kufikia makubaliano ya kikanuni na Azam FC kuhusu mchezo wao wa nyumbani dhidi ya Simba utakaochezwa Septemba 17 kuchezwa uwanja Uhuru.
TFF wamefikia makubaliano na afisa mtendaji mkuu wa Azam FC Saad Kawemba ambaye awali alikuwa ameiomba TFF kuanza kucheza michezo yake ya nyumbani dhidi ya Simba na Yanga uwanja wa Chamazi na sio uwanja wa Taifa kama ilivyo sasa.
“Azam FC wameielewa hoja ya TFF na mchezo wao dhidi ya Simba utafanyika katika uwanja wa Uhuru Septemba 17 kama kawaida saa 10 ratiba haijabadilika, makubaliano ambayo yamefikiwa na CEO wa Azam FC Saad Kawemba na katibu mkuu wa TFF Selestine Mwesigwa”
TFF imethibitisha kukubaliana na Azam FC kikanuni kucheza mchezo wake wa nyumbani Sept 17 vs Simba uwanja wa Uhuru. pic.twitter.com/g1vKAckVe4
— millard ayo (@millardayo) September 13, 2016
ALL GOALS: Simba vs AFC Leopard August 8 2016, Full Time 4-0