Arsenal imepata nguvu kabla ya dirisha la usajili la majira ya kiangazi huku ikiripotiwa kwamba nyota wa Everton Amadou Onana “huenda” akaondoka katika klabu hiyo msimu huu wa joto.
Hayo ni kwa mujibu wa Football Insider, ambayo inasema kuwa The Toffees watatafuta kati ya £50m-£60m kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 huku wakitafuta kupata faida kutoka kwa kiungo huyo.
Onana alijiunga na klabu hiyo ya Ligi ya Premia mwaka wa 2022 kama sehemu ya mkataba wa £33m na Lille ya Ligue 1 na amekua mmoja wa wachezaji bora wa Everton, ambayo imevutia vilabu kadhaa vya Ligi ya Premia.
Arsenal walihusishwa na nyota huyo wa Ubelgiji mwezi Januari, huku Chelsea, Newcastle, Manchester United na Barcelona vilabu vingine vinavyodaiwa kumtaka, liliripoti The Standard.
Kiungo ni eneo moja la uwanja ambao The Gunners watatafuta kuongeza ubora kwenye msimu huu wa joto lakini hawatataka kutumia kiasi kikubwa cha fedha kwani kipaumbele chao ni namba tisa.
£50m ni bei nzuri ya kumlipa Onana na ni pesa ambazo Everton wanahitaji kusaidia katika masuala yao ya kifedha.