Watoto zaidi ya 10 wamefariki dunia baada ya kukosa huduma ya joto katika hospitali ya Amana Jiji Dar es Salaam.
Taarifa kutoka hospitalini hapo zinaonyesha watoto hao waliozaliwa kabla ya wakati (njiti) walifariki February 16 mwaka huu.
Chanzo cha vifo hivyo kimetajwa kuwa ni uzembe wa wauguzi baada ya kukatika kwa umeme kwenye chumba walimohifadhiwa watoto hao.
“Umeme ulikatika muda wa saa 5 asubuhi hadi saa 10 jioni, wauguzi hawakutekeleza wajibu wao wa kuwaita wazazi wa watoto hao ili wawachukue kwa ajili ya kuwasaidia kupata joto, matokeo yake watoto walifariki dunia“; amesema mmoja wa wazazi waliofiwa.
Hata hivyo baadhi ya madaktari wa hospitali hiyo waligoma kuzungumzia na Gazeti la JAMHURI kuhusu suala hilo huku mganga mkuu wa Hospitali hiyo Dk. Meshack Shimwela akisema taarifa hizo si za kweli na huenda watoto hao walikufa kutokana na matizo mengine na sio umeme kwa kuwa wana jenereta za dharura.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram, na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook