Taasisi ya Flaviana Matata Foundation imekabidhi nyumba kwa Walimu wawili wa Shule ya Msingi Msinune iliyopo Kiwangwa, Chalinze Mkoani Pwani ikiwa ni utekelezaji wa awamu ya kwanza ya mradi wa ujenzi wa nyumba za Walimu shuleni hapo, na hii ni baada ya awamu ya kuboresha mazingira ya shule ya Msinune iliyojumuisha ujenzi na ukarabati wa madarasa, ujenzi wa ofisi za Walimu na vyoo kwa ajili ya Walimu na Wanafunzi, mfumo wa maji pamoja na hifadhi ya maji shuleni hapo.
Mradi huo ambao mpaka kukamilika kwake utajumuisha ujenzi wa nyumba nane za Walimu, ulianza kutekelezwa November mwaka 2019 ambapo nyumba hizo zilizokabidhiwa zina sebule, vyumba viwili vya kulala, jiko, choo na bafu asema Flaviana Matata Mwanamitindo wa Kimataifa ambaye amekua akifanya kazi na kuishi New York Marekani.
Wakati wa kukabidhi nyumba hizo kwa Uongozi wa shule ya Msingi Msinune na Serikali ya Kijiji, Muasisi wa taasisi hiyo Flaviana Matata alielezea kwamba Taasisi yake imekuwa ikishirikiana na shule ya Msinune kwa zaidi ya miaka mitano ambapo nia na madhumuni ya kujenga nyumba kwa ajili ya Waalimu ni kuhakikisha Shule inafanikiwa kuvutia Walimu wazuri ambao watakuwa wamehakikishiwa makazi bora hivyo kuchangia zaidi upatikanaji wa elimu bora na kupelekea ufaulu mzuri wa Wanafunzi.
“Ni imani yetu kwamba nyumba za walimu shuleni Msinune zitakuwa ni chachu kwa walimu wazuri kuja kufundisha shuleni Msinune hivyo kuhakikisha maendeleo mazuri ya mtoto wa kike na kuhakikisha elimu bora inatolewa kwa wanafunzi wote.” – Flaviana Matata
MAAJABU: DUKA LISILO NA MLANGO WA MBAO WALA WA CHUMA NA HAKUNA ANAYETHUBUTU KUDOKOA HATA KIBERITI, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA
EXCLUSIVE: DODOMA KAMA ULAYA STAND MPYA YA MABASI NI KAMA AIRPORT, YASHIKA NAMBA 1 TANZANIA