Halmashauri ya Jiji la Tanga limelishukuru Shirika la Amend Tanzania kwa kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi kuhusu usalama barabarani sambamba na uboreshaji wa miundombinu katika shule za Msingi hatua iliyowezesha kupunguza ajali
Elimu hiyo ilitolewa kupitia mradi wa Usalama Barabarani kupitia Tanga Yetu chini ya Ufadhili wa Shirika la Botnar Foundation ambao ulianza mwaka 2019 na kumalizika rasmi mwaka 2023 ambao umekuwa na manufaa makubwa.
Akizungumza wakati wa kuhitimisha mradi huo ambao ulianza mwaka 2019 na kumalizika mwaka 2023, naibu meya wa Jiji la Tanga Rehema Mhina amesema katika kipindi cha miaka minne wamekuwa na Amend katika kushirikiana kuhusiana na suala zima la usalama barabarani.
“Amend ni miongoni mwa mashirika yanayofanya kazi kwa ukaribu katika program ya Tanga Yetu , ni miongoni mwa miradi 17 tuliyokuwa nayo katika miradi ya Tanga Yetu na moja ya mradi huo ni mradi wa usalama barabarani.Katika mradi huu waliokuwa wamepata kazi ya kuusimamia na kuendesha ni Amend.
“Mradi huu umefika mwisho na umefanyika kwa miaka minne ukiwa unafadhiliwa na Shirika la Botnar chini ya mradi wa Tanga yetu na leo tumekuja kuwapa taarifa wadau tuliokuwa tunashirikiana nao tangu mwanzo kama.
“Ni mradi ambao umekuwa na mafanikio makubwa ndani ya miaka hii minne kwa kuhakikisha elimu ya usalama barabarani imetengamaa na imejitosheleza katika jiji letu la Tanga, kwasababu mradi huu pia uligusa uboreshaji wa miundombinu,”amesema Rehema
“Elimu hiyo imetolewa ya kutosha katika Jiji la Tanga na zimetolewa kwa nyakati tofauti lakini hawakuishia hapo wametoa elimu kwa madereva zaidi ya 900 ambao nao walipewa elimu sahihi ya matumizi ya barabara lakini jinsi gani ya kumlinda mtumia barabara ili na yeye awe salama.”
Ameongeza kikubwa zaidi ambacho Amend walikifanya na kuvutia zaidi ni kuwa kuanzisha Mahakama Kifani ya Watoto iliyokuwa ikiendesha kesi za madereva waliovunja sheria za usalama barabarani na madereva hao walihukumiwa.
Awali akizungumza katika kuhimitisha mradi huo Meneja wa Shirika la Amend Tanzania Simon Kalolo alisema mafanikio tokea kuanzishwa mradi huo mwaka wa 2019 wamefanya kazi mbalimbali ikiwemo uboreshaji wa miundombinu katika shule za msingi 11.
Alisema katika uboreshaji huo ulikuwa ni pamoja na njia za miguu, madaraja ya waenda kwa miguu, alama za barabarani, matuta, alama za pundamilia, na zaidi;
Mkurugenzi huyo alisema pia walitoa mafunzo kwa waendesha pikipiki kwa waendesha pikipiki zaidi ya 900, kwa kushirikisha Polisi wa Trafiki na viongozi wa vyama vya bodaboda;
“Lakini pia utekelezaji wa Mahakama ya Watoto katika shule tano za msingi (Usagara, Mwanzange & Martin Shamba, Mwenge, Mwakizaro),Elimu ya usalama barabarani kwa zaidi ya watoto 12,000 wa shule za msingi,Uwezeshaji wa mafunzo kwa Polisi wa Trafiki”Alisema Mkurugenzi huyo.
Alisema kwamba kampeni hiyo ya uhamasishaji wa usalama barabarani ilikuwa ikijumuisha kampeni ya vyombo vya habari, ujumbe kupitia kwa maafisa wa maendeleo ya jamii na ujumbe kupitia wanasiasa wakiwemo madiwani,
Warsha zaidi ya nane za wadau na wadau muhimu zikiwahusisha wakiwemo Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga, Mkurugenzi wa Jiji na Mkurugenzi, Kamanda wa Polisi Mkoa, Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani (RTO) na Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Barabarani.
Jumla ya maofisa wa serikali 139, taasisi za elimu 14, wanafunzi 12,894, walimu 128, askari polisi 29 na madereva 1,220 wameguswa moja kwa moja na mradi huu.
Kutengeneza Mpango Kazi wa Usafiri Salama na Endelevu wa Jiji la Tanga