Jennifer Lee Wilson (49), Mwanamke kutoka Marekani amehukumiwa kifungo cha miaka sita Jela baada ya kusababisha kifo cha Mtoto wake wa kambo wa miaka 10 Dakota Stevens kwa kumkalia kwa takribani dakika tano ambapo Mwanamke huyo mwenye uzito wa kilo 154 alidai kuwa Mtoto huyo alikuwa akikataa kufanya kazi za nyumbani na kufanya fujo siku hiyo ya tukio.
Polisi walipokea simu ya dharura kuhusu Mtoto aliyekuwa hajitambui na walipofika eneo la tukio walimkuta Dakota akiwa amelala chini karibu na Barabara ya Nyumba alikua akiishi akiwa hajitambui, hakuwa na mapigo ya moyo na alionekana na majeraha kwenye shingo na kifua ambapo alikimbizwa Hospitalini lakini alotangazwa kufariki siku mbili baadae.
Uchunguzi wa kitabibu ulionyesha kuwa kifo chake kilitokana na kukosa hewa kwa muda mrefu, kuvimba kwa ubongo na majeraha ya ndani.
Ushahidi wa kamera ya usalama ulionyesha Jennifer ambaye alikua Mama Mlezi wa Dakota akimkalia Dakota kwenye sehemu ya tumbo na shingo na kisababisha Mtoto huyo kushindwa kupumua ambapo alidai kuwa alifikiri Mtoto huyo alikuwa akijifanyisha kushindwa kupumua kabla ya kugundua kuwa hakuwa akipumua.
Mahakama imemuhukumu Mama huyo Mlezi kifungo cha miaka mitano Gerezani kwa kosa la uzembe uliosababisha kifo ambapo pia tukio hili limezua maswali kuhusu usalama wa Watoto wanaolelewa katika mazingira ya kulea nje ya Familia zao.