Katika ripoti yake, shirika la kimlataifa la haki za Binadamu la Amnesty International linashutumu Idara ya Usalama wa Ndani, ambayo iko chii ya mamlaka ya Jeshi la Taifa la Libya linaloongozwa na Marshal Khalifa Haftar, kuhusika na vifo vya watu walioko kizuizini, mauaji na watu kuwekwa kizuizini kiholela.
Ikiongozwa na Osama al-Derssi, Idara ya Usalama wa Ndani, inayoelezewa na Amnesty kama “kundi lenye silaha”, inawatia hofu wajosoaji na wapinzani, wakiwemo viongozi wa vyama vya siasa, wanaharakati, waandishi wa habari na wanablogu.
Kulingana na shirika hilo lisilo la kiserikali, makumi ya watu walikamatwa mashariki mwa Libya bila kibali na watu waliokuwa na silaha nzito.
Watu hawa wananyimwa mawasiliano na familia zao au wanasheria, wanateswa na hawahukumiwi kamwe au kufikishwa mbele ya mamlaka ya mahakama ya kiraia.