Mkurugenzi wa Mashitaka Tanzania (DPP), Biswalo Mganga amezungumzia hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambayo imewahukumu miaka 17 jela wafanyabiashara watatu.
Waliokumiwa ni Raia wa China, Yang Feng Glan ‘Malkia wa Tembo’ raia wa Tanzania ni Salvius Matembo na Philemon Manaseambapo walipatikanana hatia kwa kujihusisha na ulanguzi wa biashara haramu ya Meno ya Temboikiwemovipande 860 vyenye thamani ya Bilioni 13.
Mara baada ya hukumu hiyo, DPP Mganga alizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema Tembo ni maliasili za Tanzania na kuna watu wanakuja nchini kuwaangalia hao wanyama na kama hazijalindwa hazitakuwepo.
“Nawashukuru wadau wote kwa kuhakikisha taarifa za wahusika zimetolewa, wadau waliohusika katika upelelezi, mahakama na mawakili wa pande zote mbili waliosimamia kesi hiyo,” amesema.