Isaac Mnyagii mkazi wa kata ya sombetini katika jiji la Arusha ameachiwa kwa dhamana na mahakama ya wilaya ya Arusha baada yakukaa magereza siku 14
Mnyagi ambaye alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza may 31,2023 alikosa dhamana kwenye shtaka
La kumdhuru Jackline Mkonyi kwa kumpiga sehemu mbalimbali za mwili wake pamoja na kumg’oa jino ambapo upande wa jamhuri uliomba mahakama isimpe dhamana
Hakimu aliyekuwa akisikiliza kesi Jenipha Edward hiyo baada ya kusikiliza sababu zilizokuwa zimetolewa na pande zote mbili alisema kosa analoshtakiwa nalo lina dhamana lakini kuzingatia mazingira ya jesi anaona kumuachia inaweza kuhatarisha usalama wake
Kesi hiyo imeahirishwa na hakimu Jenipha Edward hadi june 29 itakapoanza kusikilizwa ambapo Jackline Mkonyi mlalamikaji kwenye kesi hiyo alionekana mahakamani hapo