Kiungo wa kati wa Brazil Casemiro amefichua kuwa Carlo Ancelotti alilia mbele yake baada ya kujua uamuzi wa mchezaji huyo kuondoka Real Madrid na kujiunga na Manchester United mwaka 2022.
Casemiro aliiambia El Chiringuito: “Sijamwambia mtu yeyote jambo hili hapo awali. Nilitilia shaka kuhamia kwangu Manchester mara moja tu. Nakumbuka ilikuwa Ijumaa na [uhamisho] haujakamilika isipokuwa saini. Nilikwenda kuzungumza nikiwa na Ancelotti…watu walijua kuwa imekamilika niliingia ofisini kwake na tayari alijua.
“Nilipogeuka Ancelotti alikuwa analia, nikamwambia ‘huwezi kulia mtu yeyote ila wewe’ akaniambia ‘Case sijui kwanini nalia lakini nakupenda sana. na sitaki uondoke.’
“Huo ndio wakati … nilitambua jinsi watu wengi walinipenda pale. Lakini nilikuwa tayari nimeshatoa neno langu [kuondoka] na neno langu liko juu ya kila kitu.”