Meneja wa Manchester United Erik ten Hag amekataa kumlaumu André Onana licha ya makosa mawili ya kipa wa Cameroon kuchangia sare ya 3-3 na Galatasaray siku ya Jumatano.
Matumaini ya United kufuzu kwa raundi ya muondoano yanazidi kuning’inia baada ya kuachana na mabao mawili kwa moja kwenye uwanja wa Rams Park.
Timu ya Ten Hag iliongoza 2-0 na 3-1 lakini Onana akaruhusu mikwaju ya bure ya Hakim Ziyech kila upande wa kipindi cha mapumziko kuchangia matokeo ambayo yanawaacha mkiani mwa Kundi A.
“Yuko sawa,” Ten Hag alisema.
“Kama nilivyosema, haimhusu mtu binafsi. Ni kweli makosa ya mtu binafsi kwenye soka yanaweza kuleta mabadiliko na wewe ukawajibikia, lakini kila mara ni kuhusu timu.
“Timu hii ni nzuri, wachezaji wote kikosini ni wazuri na wanastahili bora zaidi, kucheza Manchester United, kwa sababu ni wachezaji mahiri. Na hilo ni muhimu kwa kikosi kizima.”
United bado hawajaondolewa kwenye Ligi ya Mabingwa licha ya kushinda mchezo mmoja tu kati ya mitano, lakini nafasi yao ya kutinga hatua ya 16 bora ni finyu.