Dec 10 Rais wa awamu ya tano Dr.John Pombe Magufuli aliteuwa rasmi baraza la mawaziri, miongoni waliotajwa ni mbunge wa Ilemela Angelina Mabula ambaye aliteuliwa katika nafasi ya naibu waziri wa Ardhi.
Sasa mbunge huyo amefanya exclusive interview na ripota wa millardayo.com baada ya kuteuliwa katika nafasi hiyo ya kuwa naibu waziri…’Kwanza namshukuru Mungu…pili namshukuru Rais wa awamo ya tano kunichagua katika nafasi ya unaibu kwa wana ilemela niseme tu kwamba nawashukuru tu wao kwasababu wasingenipa nafasi ya ubunge nisingefika hapa nilipo kwahiyo ningependa kuwaambia kwamba tupo bega kwa bega’ – Angelina
‘Naomba nikuhakikishia kwamba mimi sio kati ya wale wanaojisahahu kwasababu dhamana hii niliyopewa ya unaibu waziri ina mikono ya wana ilemela kwahiyo niseme kwamba nitakuwa pamoja maana unapokuwa waziri au naibu waziri kuna vipindi ambavyo vipo unatakiwa kuwa jimboni…sikutarajia nafasi ya kuwa naibu waziri ila kwasababu Mh Rais kuniaminia ndio maana akanipatia hiyo nafasi’ – Angelina Mabula
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line yatiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana naMillardAyo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE