Hatua hiyo iliyopitishwa katika azimio wiki iliyopita itaruhusu kuingia bila visa kwa kukaa kwa siku 90 kwa raia kutoka zaidi ya nchi 90.
Azimio hilo jipya limo katika Amri ya Rais Namba 189/23 ya tarehe 29 Septemba 2023. Inakuja wakati nchi hiyo ya kusini mwa Afrika inafungua mipaka yake kwa wageni kutoka idadi kubwa ya nchi ili kukuza sekta yake ya utalii.
Mataifa 14 ya Kiafrika yamo kwenye orodha ya kuingia bila visa. Nchi hizo ni pamoja na Tanzania, Eswatini, Morocco, Lesotho, Rwanda, Zimbabwe, Equatorial Guinea, Botswana, Madagascar, Malawi, Mauritius, Seychelles, Cape Verde na Algeria.
Waafrika Kusini hawajahitaji visa kwa Angola tangu tarehe 1 Desemba 2017, wakati mkataba wa kukomesha visa ulipotiwa saini kati ya mataifa yote mawili.
Ni nchi tano pekee za Kiafrika (Seychelles, Msumbiji, Rwanda, Comoro na Madagaska) zinazotoa ufikiaji wa visa bila malipo au visa wanapowasili kwa raia wa nchi zote za Kiafrika. Angola ni nchi ya pili barani Afrika kwa uzalishaji wa mafuta