Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo amemuagiza Mkuu wa wilaya ya Mkuranga na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya hiyo kuanza ujenzi wa madarasa haraka iwezekanavyo katika shule ya msingi Mwandege ili kuondoa msongamano wa wanafunzi madarasani.
Agizo hilo amelitoa leo baada ya kutembelea katika Shule hiyo yenye zaidi ya wanafunzi 3700 ambapo kati yao wanafunzi zaidi ya 560 ni darasa la kwanza pekee.
Amesema kutokana na hamasa kubwa ya jamii kuwapeleka watoto kujiunga na elimu ya msingi kwa kutumia fursa ya elimu ya msingi bila malipo kumesababisha msongamano wa wanafunzi shuleni hapo.
Jafo ameagiza ujenzi wa shule mpya katika eneo la Kipara Mpaka ambalo lipo jirani na shule ya mwandege sambamba na kukamilisha shule mpya ya Chatembo ili kupunguza idadi kubwa ya wanafunzi waliopo kwenye shule hiyo.
Katika kupunguza kero hiyo ya upungufu wa nyumba vya madarasa, Waziri Jafo amewapa hamasa walimu kwamba serikali itapeleka fedha ndani ya wiki hii ili ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa uanze haraka iwezekanavyo.
“Ifikapo Machi 6, mwaka huu vyumba vya madarasa viwe vimekamilika na nawaonya Ofisi ya mkuu wa wilaya na Ofisi ya mkurugenzi kuacha malumbano yasiyo na maana ambayo yanarudisha nyumba upelekaji wa huduma za jamii kwa wananchi,” -Jafo
“Tunawatia watu umasikini, hii sio haki” –Hussein Bashe