Nahodha wa timu ya taifa ya Ureno na mshambuliaji wa Real Madrid ya Hispania Cristiano Ronaldo amerudi kwanye headlines tena baada ya kuja na application yake, Ronaldo ameamua kuanzisha application yake ya kupiga selfie na mashabiki wake sio lazima kuonana nae.
Application hiyo inayotumia jina la kibiashara la staa huyo inaitwa CR7 Selfie inapatikana katika play store tayari na gharama ya kununua application hiyo ni dola 2.22, lengo la Ronaldo kuanzisha application hiyo ni kuchangisha pesa kwa ajili ya watoto wakimbizi.
Kama utakuwa unakumbuka vizuri brand ya Cristiano Ronaldo inazidi kukua siku hadi siku, Ronaldo tayari ameingia katika masuala ya fashion na brand hiyo, mavazi ya kuogelea na biashara za hotel ambazo zote zinatumia jina hilo hilo la CR7.
ALL GOALS: Simba vs AFC Leopard August 8 2016, Full Time 4-0