Khatija Juma (15) mwanafunzi wa Kidato cha Tatu shule ya Sekondari Ndono Mkoani Tabora anatarajia kuiwakilisha Tanzania katika mashindano la TEHAMA kwa mtoto wa kike kati ya miaka 13-19 litakalofanyika April 25 nchini Ethiopia katika kongamano la TEHAMA duniani, baada ya kubuni Application itakayomsaidia Mama mjamzito kupata huduma ndani ya wakati.
“Application yangu inaweza kuwasaidia akinamama na mama akiwa anatumia hiyo application itakuwa na uwezo wa kumkumbusha siku fulani anatakiwa aende cliniki na kama hajawahi kwenda cliniki hana uwezo wa kutumia ina warning kabisa, mtu atajisajili kama anavyoweza kujisajili Whatsap au Facebook” Khatija Juma