July 3, 2017 stori nyingi zimeripotiwa kwenye Televisheni, Radio, Magazeti na Mitadao mbalimbali na miongoni mwa stori hizo ni issue ya Rais Magufuli kuweka jiwe la msingi kuzindua mradi wa ujenzi, upanuzi na ukarabati wa Bandari ya DSM.
Nimekukusanyia na kukusogezea karibu stori zote kubwa asubuhi ya leo kupitia millardayo.com.
"Tanzania leo hakuna uhuru wa watu kutoa na kupokea habari kama Katiba yetu inavyotaka." – Frederick Sumaye. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) July 3, 2017
Watoto 24 waliozaliwa na matatizo ya usikivu (viziwi) watafanyiwa upasuaji wa kupandikizwa vifaa vya usikivu kila mwaka Muhimbili #MTANZANIA
— millardayo (@millardayo) July 3, 2017
Waziri Mkuu wa zamani Sumaye amesema Katiba mpya imewekwa pembeni kwa kuwa watawala hawataki madaraka yao yadhibitiwe na Katiba. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) July 3, 2017
Wabunge wameitaka Serikali kueleza maandalizi yake kwenye ulinzi wa hifadhi ya madini itakayokuwa Bank Kuu (BoT) kabla ya kuyauza. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) July 3, 2017
Mahakama ya Wilaya ya Mlele, Katavi imemhukumu mfungwa Juma Masasila (38) miaka 40 zaidi jela kwa kumiliki nyara za serikali. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) July 3, 2017
Muuguzi wa Hospitali ya Rufaa Geita amepigwa faini ya Tsh. 200m kwa kutumia lugha ya kashfa kwa watumishi wa Hospitali ya Makoye. #MWANANCHI
— millardayo (@millardayo) July 3, 2017
Rais Magufuli amewaonya wanasiasa wanaozungumza kuhusu watu waliokuwa mahabusu kukaa kimya wakati serikali inafanya kazi yake. #MWANANCHI.
— millardayo (@millardayo) July 3, 2017
CHADEMA Arusha imewataka viongozi wanaotaka kuhama wafanye hivyo haraka kwa kuwa chama kina kazi zinazohitaji kujitoa kwa dhati. #MWANANCHI.
— millardayo (@millardayo) July 3, 2017
Mkuu wa Wilaya ya Tarime Glorious Luoga amewaonya waajiri waache kuwanyanyasa waajiriwa ktk mishahara na mikataba ya kazi. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 3, 2017
Mahakama ya Wilaya ya Maswa, Simiyu imemhukumu Elisha Edward miaka 30 jela kwa kosa la kumbaka na kumpa ujauzito mwanafunzi. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 3, 2017
Mbunge wa zamani wa Kigoma Mjini David Kafulila amesema Bajeti 2017/18 haitatekelezeka kama nchi itaendelea kukosa mikopo. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 3, 2017
Taasisi ya Tanzania Mzalendo Foundation imemtaka Spika Ndugai kusimamia haki na usawa Bungeni na kuheshimu mihimili mingine. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 3, 2017
Jeshi la Polisi Kilimanjaro limefanikiwa kumkamata Afisa wake aliyekuwa anasakwa kwa tuhuma za kujihusisha na wizi wa magari. #TanzaniaDAIMA
— millardayo (@millardayo) July 3, 2017
Jeshi la Polisi Tabora linamshikilia Halid Mohamed (28), mkazi wa Igunga kwa tuhuma za kulawiti wananfunzi wawili wa Shule ya Msingi. #UHURU
— millardayo (@millardayo) July 3, 2017
DC Bagamoyo Alhaj Mwanga ametoa rai kwa wanawake nchini kuchangamkia fursa za viwanda ili kupata soko na kuondokana na umasikini. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) July 3, 2017
ADA Tadea imewataka wanasiasa na viongozi wastaafu wa Serikali kuacha tabia inayokuza mipasuko ya jamii katika shutuma za uhalifu. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) July 3, 2017
Wakurugenzi na Wakuu wa Wilaya wameagizwa kuwachukulia hatua wasiofanya usafi ktk mazingira na watupa taka ovyo kwa kukiuka sheria. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) July 3, 2017
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) imeagizwa kupeleka wahandisi wa kutosha ktk ujenzi wa gati ya Mtwara ili kupata uzoefu. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) July 3, 2017
Polisi Shinyanga wamewahoji watu watatu wanaodaiwa kumtishia maisha Mwenyekiti wa CCM Kata ya Mwakata, wilayani Kahama. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) July 3, 2017
Imeelezwa kuwa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha imeshindwa kufanya vikao vyake kusikiliza kesi zilizopo kutokana na kukosa fedha. #HabariLEO
— millardayo (@millardayo) July 3, 2017
Bandari ya DSM inatarajia kuongezewa uwezo wa kupokea meli kubwa na mizigo kutoka tani 18m hadi tani 28m ndani ya miaka 7 ijayo. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) July 3, 2017
Serikali imezitaka Taasisi za elimu ya afya na mashirika yanayofanya tafiti kuhakikisha tafiti zinawafikia wadau ili zilete tija. #HabariLEO
— millardayo (@millardayo) July 3, 2017
Mamlaka zinazohusika na ithibati zimeagizwa kutowakatisha tamaa watu wanaotaka kuanzisha viwanda kwa vikwazo visivyo na msingi. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) July 3, 2017
Watu wawili akiwemo mwanafunzi wa Form 3 wakazi wa Igunga, Tabora wamekufa maji ktk bwawa Mwanzugi baada ya mtumbwi wao kuzama. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) July 3, 2017
Waziri Mkuu Majaliwa amezindua Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini, TRURA ikiwa ni mapinduzi na dhamira ya kuboresha maisha. #HabariLEO
— millardayo (@millardayo) July 3, 2017
Wasomi UDSM wamependekeza sheria mpya ya madini iwabane wawekezaji kutumia Bank na kampuni za bima za ndani ili kukuza uchumi. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) July 3, 2017
Majibu ya Rais Magufuli kwa wanasiasa wanaotetea wahalifu!!!