Jumapili ya January 1 2017 Ligi Kuu England msimu wa 2016/2017 iliendelea kwa michezo miwili kuchezwa katika kiwanja wa cha Emirates na kiwanja cha Vicarage kinachotumiwa na Watford kama uwanja wao wa nyumbani.
Kwa upande wa uwanja wa Emirates Arsenal waliwakaribisha Crystal Palace kucheza nao mchezo wa 40 katika historia ya vilabu hivyo toka walipokutana kwa mara ya kwanza 27 Jan 1934 katika mchezo wa FA Cup, Arsenal wakiwa nyumbani walipata ushindi wa goli 2-0, magoli yakifungwa na Oliver Giroud dakika ya 17 na Alex Iwobi dakika ya 56.
Goli la kwanza la Arsenal lililofungwa na mfaransa Oliver Giroud ndio lilikuwa kivutio na stori kubwa kwa wapenzi wa soka la England, kwani lilionekana kulijadili zaidi katika mitandao kutokana na style yake lilivyofungwa na kufananishwa na lile la Henrikh Mkhitaryan wa Man United alilofunga dhidi ya Sunderland.
Goli la Oliver Giroud aliloifungia Arsenal Jan 1 katika ushindi wa 2-0 vs Crystal Palace, limekuwa likijadiliwa sana mitandaoni. pic.twitter.com/xWG1c0lEr4
— millard ayo (@millardayo) January 1, 2017
ALL GOALS: JKT Ruvu vs Yanga December 17 2016, Full Time 0-3