January 5 2017 Abuja Nigeria ndio ilifanyika hafla ya utolewaji wa tuzo za soka za mwaka 2016 na shirikisho la soka barani Afrika Caf, tuzo hizo ambazo utolewa kwa wachezaji waliyofanya vizuri kwa mwaka husika kwa kupigiwa kura, staa wa timu ya taifa ya Algeria na timu ya Leicester City ya England Riyad Mahrez alitangazwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora Afrika.
Mahrez alitangazwa kushinda tuzo hiyo kwa kura 361, huku Pierre-Emerick Aubameyang akishika nafasi ya pili kwa kupata kura 313 wakati Sadio Mane wa Liverpool amemaliza nafasi ya tatu kwa kupata kura 186.
Tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wa ndani ambayo alishinda mtanzania Mbwana Samatta kwa mwaka 2015, safari hii imerudi tena Afrika Mashariki kwa golikipa wa Mamelodi Sundowns na timu ya taifa ya Uganda Denis Onyango kushinda tuzo hiyo.
Riyad Mahrez wa Algeria na Leicester City ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika 2016 amewashinda Mane na Aubameyang #CAFawards pic.twitter.com/evHd7HD53b
— millard ayo (@millardayo) January 5, 2017
Wachezaji 11 waliyofanikiwa kuunda kikosi bora cha Afrika kwa mwaka 2016 #CafAwards Africa Finest XI pic.twitter.com/lZJupWTyRX
— millard ayo (@millardayo) January 5, 2017
Golikipa wa Uganda na Club ya Mamelodi Sundowns Denis Onyango ameshinda tuzo ya mchezaji bora Afrika kwa Ligi za ndani #CafAwards pic.twitter.com/s9gURSuR3Y
— millard ayo (@millardayo) January 5, 2017
Bakary Papa Gassama wa Gambia ameshinda tuzo ya refa bora wa mwaka 2016 #CafAwards pic.twitter.com/vrcHaBC8cD
— millard ayo (@millardayo) January 5, 2017
Mchezaji wa Nigeria Asisat Oshoala ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa kike kwa mwaka 2016 #CafAwards pic.twitter.com/bghtkWbt7T
— millard ayo (@millardayo) January 5, 2017
Uganda The Cranes imeshinda tuzo ya timu bora ya taifa ya wanaume kwa mwaka 2016 #CafAwards pic.twitter.com/ROBtXdW134
— millard ayo (@millardayo) January 5, 2017
Kocha wa Mamelodi Sundowns Pitso Mosimane ameshinda tuzo ya kocha bora wa mwaka 2016 #CafAwards pic.twitter.com/5Q0ISFPojt
— millard ayo (@millardayo) January 5, 2017
Staa wa Arsenal na Nigeria Alex Iwobi ameshinda tuzo ya mchezaji bora kijana kwa mwaka 2016 #CafAwards pic.twitter.com/MgUekP1buQ
— millard ayo (@millardayo) January 5, 2017
Staa wa ManCity na timu ya taifa ya Nigeria Kelechi Iheanacho ameshinda tuzo ya Most Promising talent 2016 #CafAwards pic.twitter.com/wzA4SlfmET
— millard ayo (@millardayo) January 5, 2017
Mabingwa wa Club Bingwa Afrika Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini wameshinda tuzo ya Club bora ya mwaka 2016 #CafAwards pic.twitter.com/RDkwT9YiPr
— millard ayo (@millardayo) January 5, 2017
Timu ya taifa ya wanawake ya Nigeria imeshinda tuzo ya timu bora ya mwaka 2016 ya wanawake #CafAwards pic.twitter.com/i0pfyVtSc2
— millard ayo (@millardayo) January 5, 2017
ALL GOALS: JKT Ruvu vs Yanga December 17 2016, Full Time 0-3