Rais wa Marekani, Donald Trump Leo January 31, 2018 amelihutubia taifa hilo kwa mara ya kwanza tangu achaguliwe kuwa Rais ambapo amewataka Wamarekani wazingatie umoja wa kitaifa, mipaka yenye uthabiti na uwezo mkubwa wa kijeshi.
Trump ametia saini amri mpya kwa ajili kuliendeleza gereza la Guantanamo, hatua ambayo imebatilisha uamuzi rasmi wa mtangulizi wake Barack Obama aliyefanya jitihada za miaka minane kwa ajili ya kulifunga gereza hilo. Jambo hilo lilikuwa ni moja kati ya ahadi alizozitoa Trump wakati wa kampeni alisema anataka jela ya Guantanamo ibakie wazi na itumiwe kwa kuwazuia watu wabaya, japokuwa yeye mwenyewe bado hajampeleka mtu yeyote kwenye jela hiyo.
Trump alitia saini amri hiyo kabla ya kutoa hotuba yake ya kwanza kwa taifa la Marekani ambapo amesema Marekani bado ina uwezo wa kuwazuia maadui kwa kuwaweka kwenye jela hiyo ya Guantanamo iliyopo nchini Cuba kwa ajili ya kulinda usalama wa taifa la Marekani.
JPM AKIHUTUBIA KWENYE UZINDUZI WA HATI YA KUSAFIRIA YA KIELEKTRONIKI, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUMTAZAMA