Staa wa Juventus ya Itali Paulo Dybala afunguka ukweli kuhusiana na Cristiano Ronaldo wanavyomchukulia katika taifa la Lionel Messi nchinj Argentina.
Dybala afunguka hayo akihojiwa na chama cha soka cha Argentina, mara nyingi Ronaldo amekuwa akitafsiriwa tofauti na watu mitandaoni kutokana na tabia yake ya kupenda kujikubali.
”Nilimwambia kuwa Cristiano (Ronaldo) nchini Argentina tunakuchukia kidogo sababu ya umbo lako, namna ulivyo na unavyotembea, ukweli ni kwamba umenishangaza nimekukuta ukiwa tofauti na matarajio” >>> Dybala
Paulo Dybala ni miongonj mwa wachezaji wachache duniani ambao wamebahatika kucheza na mahasimu wote wawili Cristiano Ronaldo na Lionel Messi ambao hadi leo huwa mabishano juu ya ubora wao yanashamiri mitandaoni.