Bado michuano maalum ya Copa America 2016 ambayo inatumika kama kusherehekea miaka 100 ya mashindano hayo inaendelea, kama ulikuwa hujui alfajiri ya June 11 Argentina ilicheza dhidi ya Panama katika mchezo wake wa pili wa Kundi D.
Katika mchezo huo Argentina walifanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 5-0, ushindi ambao ulipatikana baada ya nahodha wao Lionel Messi kuingia katika mchezo huo dakika 29 za mwisho, kuingia kwa Messi kulikuwa kuna madhara makubwa kwa Panama, kwani ilionekana mabeki wao kushindwa kumdhibiti staa huyo.
Messi ndio mchezaji aliyesababisha kuidhoofisha zaidi Panama, kwani uwepo wake uwanjani ulifanya apachike magoli matatu yaani hat-trick dakika ya 68, 78 na 87, baada ya Nicolas Otamendi kupachika goli la kwanza dakika ya 7 na Sergio Aguero kuhitimisha furaha ya waargentina baada ya kupachika goli la mwisho dakika ya 90.
Hata hivyo Panama walilazimika kumalizia dakika 59 za mchezo kwa kucheza wakiwa na wachezaji 10 uwanjani, hiyo inatokana na mchezaji wao mmoja Anibal Godoy kuoneshwa kadi ya pili ya njano dakika ya 31 na kutolewa nje ya uwanja kutokana na kucheza faulo akiwa tayari alionywa kwa kadi ya kwanza ya njano.
Video ya magoli mechi ya Argentina vs Panama June 11 2016, Full Time 5-0
https://youtu.be/FkuMcKHm6TM
ALL GOALS: TAIFA STARS VS MISRI JUNE 4 2016, FULL TIME 0-2
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE