Najua mtu wangu wa nguvu tayari umetazama mechi za Euro 2016 zilizochezwa June 18, lakini usisahau kuwa alfajiri ya June 19 usisahau kuwa michuano maalum ya maadhimisho ya miaka 100 ya Copa America imeendelea tena kama kawaida, michuano hiyo imeendelea katika hatua ya robo fainali kwa Argentina kucheza dhidi ya Venezuela.
Argentina wamefanikiwa kuingia nusu fainali kwa kuifunga Venezuela kwa jumla ya goli 4-1, magoli ya Argentina yalifungwa na Gonzalo Higuan dakika ya 8 na 29, Lionel Messi dakika ya 60 na goli la mwisho lilifungwa dakika ya 71 na Erik Lamela, wakati Venezuela goli lao la kufutia machozi lilifungwa na Jose Rondon dakika ya 70.
Huu ni mchezo ambao Argentina alikuwa anapewa nafasi kubwa ya kushinda kutokana na rekodi yake dhidi ya Venezuela, Argentina ndani ya miaka 60 kamfunga Venezuela mara 21 wakati Venezuela amewahi kumfunga Argentina mara moja tu October 11 2011 kwa goli 1-0, lakini ndani ya miaka hiyo 60 hawajawahi kutoka sare.
Video ya magoli ya Argentina vs Venezuelea June 19 2019
ALL GOALS: Yanga vs Al Ahly (Full Time 1-1) April 9 2016 CAF
https://youtu.be/VSM0_i0-DY0
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE