Wavuvi na wafanyabiashara katika soko la Kunduchi wametakiwa kuhakikisha kuwa wanatunza vifaa vya usafi walivyokabidhiwa kwa faida yao na wakazi takribani 3,000 wanaozunguka soko hilo.
Soko la samaki la Kunduchi ndilo kubwa katika Wilaya ya Kinondoni likiwa na uwezo wa kuhudumia wateja 250-300 kwa siku kutoka maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki mara baada ya hafla ya makabidhiano ya mradi huo wenye thamani ya Milioni Tisa (9), Katibu Tawala wa Wilaya ya Kinondoni, Stella Msophe amesema ni wajibu kwa jamii ya wavuvi waishio eneo hilo kuendelea kuutunza mradi huo kwa muda mrefu ujao.
Mradi huo umetekelezwa na shirika lisilo la kiserikali la Aqua-Farms Organisation (AFO) kwa kushirikiana na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa ufadhili wa shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO).
“Nitoe rai kwa jamii ya wavuvi waishio eneo hili kuendelea kuutunza na kuulinda mradi huu ili uweze kuhudumia watu wengi zaidi na kuleta matokeo chanya ambayo yatakuza ufahamu wa namna bora ya kutunza afya zetu kwani afya ni uhai,’’ Bi Msofe.
“Nawapongeza wote waliofanikisha mradi huu kukamilika kwani utaongeza pia ubora wa mazao ya samaki katika soko hili na hivyo kuchochea biashara yenye hadhi inayotakiwa kitaifa na kimataifa,” Bi Msofe
Kwa upande wake, Bi. Grace Kakama ambaye ni Afisa uvuvi Manispaa ya Kinondoni amesema kama Wilaya wanayo furaha na mradi huo katika wilaya hiyo kwani unakwenda kuleta mapinduzi katika swala zima la usafi wa mazingira.
“Usafi wa mazingira katika mwalo huu utamuhakikishia usalama mlaji wa mwisho na pia kupunguza kwa kiasi kikubwa magonjwa ambayo yangeweza kuathiri uchumi wa nchi na mwananchi mmoja mmoja,” Bi Kakama
Kama mmoja wa viongozi, aliahidi kushirikiana na jamii ya wavuvi katika eneo hilo kuhakikisha mradi huo unatunzwa na kulindwa ili uweze kuleta matokeo chanya kwa kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.
Kwa niaba ya wenzake, Mwenyekiti wa soko hilo la samaki, Bw. Zedi Mwinyi Zedi aliahidi kuhakikisha kuwa mradi huo unadumu.
GWAJIMA AMUACHA HOI MAGUFULI KWA VICHEKO, MAGUFULI HOI, UMEWAGEUZA CHINI JUU, MBWA ACHA WABWEKE