Hii stori imeandikwa na Magazeti mengi ya leo, inahusu tukio la mwanafunzi mmoja wa kike kubakwa Arusha na mtu ambaye anaitwa Raphael au jina maarufu ‘Osama‘, mtu huyo amedaiwa ni Askari.
Ripota wa millardayo.com kampata Kamanda wa Polisi Arusha, Liberatus Sabas na kathibitisha tukio hilo.
Sentensi ya kwanza ya RPC hii hapa >>“Kuna tuhuma za Askari wangu kumbaka binti mmoja anaitwa Mwanahamisi, mashtaka ya kijeshi yameendeshwa na nimemfukuza kazi leo…“
Ya pili hii hapa >> “Baada ya kumsikiliza, tumejiridhisha kwamba ana kesi ya kujibu, tumemfukuza kazi na anapelekwa Mahakani…“- Kamanda Liberatus Sabas.
Maneno mengine ya Kamanda haya hapa >> “Jeshi la Polisi halimfungii macho mtu anayekosea, ukikosea tunakushughulikia hatukucheleweshi… mshahara wa dhambi ni mauti, tumemfukuza kazi na atasimama Mahakamani.”- Liberatus Sabas.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.