Arsenal lazima iongeze kiwango kingine msimu huu ikiwa wanataka kushinda Ligi ya Premia baada ya kukosa mara mbili, meneja Mikel Arteta alisema kabla ya mechi ya kwanza ya Ligi Kuu ya timu yake dhidi ya Wolverhampton Wanderers Jumamosi.
Kikosi cha Arteta kilimaliza na pointi 89 msimu uliopita na kufunga mabao mengi na kufungwa machache kuliko katika kampeni za awali lakini kwa mara nyingine kilimaliza washindi wa pili nyuma ya Manchester City.
“Vunja zaidi ya rekodi hizo tena na ujishindie pointi zaidi ambazo ni hakika,” Mhispania huyo aliwaambia wanahabari Ijumaa alipoulizwa ni nini Arsenal wanahitaji kufanya msimu huu ili kushinda taji.
“Haitatosha (viwango vya msimu uliopita). Kwa kiwango tunachoshindana nacho, na kila msimu unazidi kuwa mgumu, itabidi tuboreshe tena hilo ni hakika.”
Arsenal walichukua kinyang’anyiro hicho hadi siku ya mwisho msimu uliopita na wanapigiwa upatu kukomesha ubabe wa City wakati huu na kukizuia kikosi cha Pep Guardiola kushinda taji la tano mfululizo.