Arsenal wanakaribia kuinasa saini ya kiungo wa kati wa Real Sociedad Mikel Merino, kwa mujibu wa Relevo.
Inaripotiwa kwamba makubaliano sasa “yamekaribia” baada ya makubaliano yenye thamani ya Euro milioni 30 pamoja na motisha kufikiwa kati ya vilabu vyote viwili, huku The Gunners wakiwa wamepania kushinda ushindani kutoka kwa Barcelona pamoja na Atlético Madrid kuinasa saini yake.
Meneja Mikel Arteta anasemekana kuwa na jukumu muhimu katika hatua hiyo baada ya kuwasiliana na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 mara kadhaa baada ya kumtambua kama kiungo muhimu katika kikosi chake msimu huu wa joto.
Merino, ambaye aliichezea Uhispania mara saba kwenye Mashindano ya UEFA, anaaminika kuwa tayari ameshatoa mwanga kuhusu masuala ya kibinafsi kabla ya pendekezo lake la kuhamia Emirates Stadium, huku hatua hiyo ikitarajiwa kutangazwa siku zijazo.