Zubimendi, ambaye alilengwa na Real Madrid na Barcelona hapo awali, anaibuka kama chaguo la Arsenal kabla ya dirisha la usajili la Januari huku wakipania kuimarisha safu yao ya kiungo.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 amepewa kandarasi na Sociedad hadi 2027 na ana kifungu cha kutolewa cha €50m (£43.6m).
Zubimendi hakuwa mchezaji pekee aliyevutiwa na Arsenal, huku Benfica pia wakiwachezesha Joao Neves na Florentino Luis – wachezaji wawili ambao wamewatazama hapo awali.
Bayern Munich, Borussia Dortmund na Paris Saint-Germain pia walikuwepo Jumatano.
kulingana na ripoti za jarida la 90 mntszinasema kuwa Bayern haswa walikuwa kwenye mchakato huo kwa sababu sawa na Arsenal, wakiwaangalia Zubimendi na Neves, ambao wamekuwa wakiwafuatilia kwa muda mrefu.