Bayern Munich huenda ikamnunua mshambuliaji chido Obi Martin kutoka Arsenal msimu huu wa joto, gazeti la Daily Telegraph limeripoti.
Obi Martin,16, alifunga mabao saba kwa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 18 katika ushindi wao wa 9-0 dhidi ya Norwich City Jumamosi.
Fowadi huyo mzaliwa wa Denmark, amewakilisha Denmark na Uingereza katika ngazi ya kimataifa ya vijana, na pia anastahili kuiwakilisha Nigeria kupitia baba yake. Hadhi hiyo ya mataifa mawili inaweza kutumiwa vibaya na vilabu katika Umoja wa Ulaya, ambavyo vinaweza kuwapa wachezaji wachanga kandarasi za kitaaluma wakiwa na umri wa miaka 16, mwaka mmoja kabla ya vilabu vya Uingereza kufanya hivyo kisheria.
Gazeti la Telegraph linasema kuwa Bayern ni miongoni mwa vilabu vinavyomtaka Obi Martin, ambaye alitangaza habari mwishoni mwa juma kwa kupachika mabao saba. Alifunga mabao matano katika kipindi cha kwanza — akifunga la kwanza hat trick zake mbili katika dakika 17 za kwanza za mchezo — na kuongeza mengine mawili baada ya mapumziko na kufikisha mabao 24 katika mechi saba zilizopita.
Hata hivyo, hilo si jambo kubwa zaidi kwa mshambuliaji huyo msimu huu. Mnamo Novemba, alifunga mabao 10 katika mechi moja ya U16 ya Arsenal katika ushindi wa 14-3 dhidi ya Liverpool.