Arsenal wako tayari kusikiliza ofa kutoka kwa vilabu vinavyotaka kumsajili mshambuliaji Gabriel Jesus, limesema Football Insider.
Jesus, 27, amekuwa na jeraha msimu huu na ana mabao manane pekee katika mechi 33 alizocheza.
The Gunners wamekuwa wakitafuta kuboresha chaguzi zao na wanaweza kuongeza ada nzuri ya uhamisho kwa kumruhusu mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil kusonga mbele.
Gazeti la Daily Express linadai kwamba huenda kuhamia Saudi Arabia kukiwa na faida kubwa, huku ligi pia ikitaka kumleta kiungo wa kati Thomas Partey mwenye umri wa miaka 30.