Nimeona nikusogezee moja kati ya rekodi ambazo klabu ya Arsenal iliwahi kuziweka mwaka 2004 chini ya kocha Arsene Wenger ambaye yupo hadi sasa akiifundisha klabu hiyohiyo… Wenger bado ana heshima ya kipekee Emirates licha ya kuwa kwa miaka ya hivi karibuni hajaleta mafanikio makubwa kwenye Klabu hiyo.
May 2004 waratibu wa Ligi Kuu Uingereza walilazimika kutengeneza Kombe maalum la Ligi Kuu kwa ajili ya Klabu ya Arsenal, hiyo ilifanyika baada ya Arsenal kuandika rekodi ya kumaliza msimu bila kufungwa hata mechi moja msimu wa 2003-04.
Upekee wa Kombe walilopewa Arsenal msimu huo ilitokana na Bodi ya Ligi Kuu kuandaa Kombe lenye material ya dhahabu, hii ilikuwa tofauti kabisa na haikuwahi kufanyika kitu cha aina hiyo siku za nyuma na halikuwahi kutolewa Kombe la aina hiyo tena mpaka sasahivi.
Hata hivyo huo ulikuwa ni wakati ambao kikosi cha Arsenal kilikuwa kikibebwa na mastaa kama Thierry Henry, Patrick Vieira, Dennis Bergkamp, Nwankwo Kanu, Robert Pires, Ryan Smith, Sol Campbell na Reyes na wengine wengi huku makocha wakiwa Arsene Wenger na msaidizi wake Boro Primorac.
Hii ndio Video inayoonesha jamaa walivyoupata huo ushindi wao 2004.
https://youtu.be/IdIcxKdTDSQ
Nitakutumia stori zote ukibonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.