Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe Emmanuela Kaganda amewapongeza wakuregenzi wa Halmashauri za Meru na Arusha ,wataalamu na wananchi kwa ujumla kwa kushiriki kikamilifu katika mbio za Mwenge wa Uhuru ambapo miradi 16 yenye thamani ya Bilioni 17.26 imekidhi vigezo katika mbio hizo za mwenge wa Uhuru.
Ikumbukwe
Mbio za Mwenge wa uhuru katika Wilaya ya Arumeru zilikimbizwa umbali wa km 204.3 ikiwa ni tarehe 28.6.2023 ya Wilaya ya Arusha na tarehe 29.06.2023 Halmashauri ya Meru.
Pamoja na kutembelea miradi hiyo pia kwa kuzingatia muongozo wa mbio za mwenge katika kufanya vipimo vya vvu , malaria pamoja na uchangiaji wa damu.
Kwa kumalizia mkuu wa wilaya ya meru amewapokeza wakurugenzi watendaji katika halmashauri zote mbili ya Arusha pamoja na arumeru kwa kazi kubwa walioifanya ya kutekeleza miradi ya maendeleo.