Mlipuko wa bomu kwenye mji wa Arusha kwenye bar iitwayo Arusha Night Park Mianzini April 13 2014 umesababisha watu 15 kujeruhiwa na kulazwa katika hospitali tatu tofauti mkoani humo.
Waziri wa mambo ya ndani amethibitisha kujeruhiwa kwa watu lakini hakuna kifo kilichotokana na mlipuko huo ambao uchunguzi wa awali umeonyesha ni wa bomu la kutengeneza kwa mkono.
Waziri anasema >> ‘Mshambuliaji alilitengeneza kwa kuchukua chupa ya Whisky iliyotumika na kuweka utambi na vitu vingine kisha mfuko wa plastick wenye misumari alafu akalitegesha ndani ya Bar hiyo iliyokua imejaa watu wakitazama mpira saa mbili usiku’
Unaambiwa kabla ya bomu kulipuka, alietegesha bomu hilo ambae mpaka sasa uchunguzi ukiendelea hajafahamika, alihamia kwenye Bar ya jirani iitwayo ‘Washington’ na kutegesha bomu jingine la kienyeji ambalo hata hivyo halikulipuka.
Wahudumu wa bar ya ‘Arusha night park’ wamesema wakati wa mlipuko huo waliona kwanza mwanga mkubwa na moshi kujaa ambapo wenzao wameumia sana ikiwemo kuvunjika miguu huku wateja baadhi wakiumia pia walipojaribu kukimbia kutoka kwenye eneo la tukio.