Leo February 12, 2018 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbalawa ameifungua Reli ya kati ambayo haikufanya kazi takribani mwezi mmoja baada ya kuaribiwa na mafuriko ya mvua hasa maeneo ya Kilosa Morogoro.
Mbali ya kuifungua reli hiyo, pia Prof Mbalawa amesema serikali imepoteza takribani Bilioni 5 katika kipindi cha mwezi mmoja kuanzia January 11, 2018 ambapo usafiri huo ulisitishwa.
“Serikali imejipanga kuhakikisha tatizo hili linapata ufumbuzi wa kudumu, tutahakikisha njia ya Reli inapanda juu au tutahamisha hii reli, lazima tutafute suluhisho la kudumu, mapato ambayo kwa mwezi mmoja Reli hii imepoteza ni zaidi ya Bilioni 4” -Prof. Mbalawa
“NAWATAKIA KAZI NJEMA, KAFANYENI KAZI” -RAIS MAGUFULI, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA