Kampuni ya Asas Dairies leo August 26, 2023 imezindua Program ya Unywaji wa Maziwa Mashuleni mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi ambae ameonyesha kufurahishwa na program hiyo.
Mkurugenzi wa Asas Dairies Bw. Ahmed Salim Asas amemueleza Rais Mwinyi kuwa kwa kuanzia wamepanga kugawa zaidi ya Lita 5,000 kwenye Shule zaidi ya 25 Zanzibar.
Aidha amesema hatua hiyo imekuja kufuatia ripoti ya mwaka jana iliyotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu kuonyesha asimia 1.8 ya watoto Zanzibar wana tatizo la Udumavu jambo lililowalazu Kushirikiana na Wizara ya Afya na Wizara ya Elimu kupunguza na ikiwezekana kumaliza tatizo Hilo.
Pamoja na Hiyo amesema lengo lingine la program hiyo ni kuimarisha lishe na Afya za Wanafunzi Mashuleni na Wananchi kwa ujumla.
Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), kwa mwaka mtu Mmoja anatakiwa kunywa Maziwa yasiyopungua Lita 200 lakini kwa Sasa takwimu zinaonyesha Hali ya Unywaji maziwa Nchini sio ya kuridhisha.