Ni Agosti 15, 2023 ambapo Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Njombe ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mheshimiwa Kissa Gwakisa Mkuu wa Wilaya ya Njombe imefnaya ziara katika kampuni ya ASAS mkoani Iringa, ambapo imetembelea kiwanda cha Maziwa cha kampuni ya ASAS pamoja na Shamba la Mifugo.
Mkurugenzi wa kiwanda cha maziwa ya ASAS Ndg. Ahmed Abri amekusudia kufungua kiwanda chenye uwezo wa kuchakata maziwa lita elfu 50 kwa siku moja wilaya ya Njombe.
Ameyasema hayo akiwa na kamati ya Usalama ya wilaya ya Njombe ikingozwa na Mkuu wa wilaya hiyo Mhe. Kissa Kasongwa mara baada ya kupata mwaliko wa kutembelea kiwanda cha uzalishaji maziwa kilichopo mkoani Iringa na shamba la Mifugo.
Mkurugenzi huyo amesema licha ya uwekezaji wa kiwanda hicho pia watatoa mkopo wa Ng’ombe wa maziwa kwenye vikundi vya wafugaji wilayani Njombe na kueleza kuwa uwekezaji huo utaanza mara moja pindi tu ardhi ikipatikana.
Mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa amesema mpaka sasa Halmashauri ya Mji ya Njombe inaendelea na zoezi la kuhakikisha ardhi inapatikana ili kufanikisha lengo la muwekezaji huyo na kueleza kuwa kiwanda hicho kitaleta tija kwa wafugaji na kitasaidia kupunguza tatizo la utapiamlo.