Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeahirisha kesi ya uhujumu uchumi na kuisababishia hasara serikali ya Sh.bilioni 2.4 inayomkabili Mkurugenzi wa Tathmini ya Madini, Archard Kalugendo (49) hadi January 3,2018 kwa sababu upelelezi haujakamilika.
Mbali ya Kalugendo, mshtakiwa mwingine ni Mthamini wa Madini ya Almasi wa Serikali, Edward Rweyemamu (50).
Kesi hiyo imeahirishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Respicious Mwijage baada ya Wakili wa serikali, Esther Martin kueleza kuwa shauri hilo limeitishwa kwa ajili ya kutajwa na upelelezi wake haujakamilika.
Kutokana na taarifa hiyo, Hakimu Mwijage ameahirisha kesi hiyo hadi January 3,2018.
Kwa pamoja washtakiwa wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi kwa kuisababisha serikali hasara ya zaidi ya Sh.bilioni 2.
Inadaiwa kuwa kati ya August 25 na 31, 2017 katika maeneo mbalimbali kati ya Dar es Salaam na Shinyanga, washtakiwa hao kwa pamoja na kwa vitendo vyao wakiwa wathamini walioajiriwa na Wizara ya Nishati na Madini waliisababisha serikali hasara ya kiasi hicho cha fedha.
MAAMUZI YALIYOTOLEWA NA MAHAKAMAKUU KWA BODI YA PROF. LIPUMBA, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA