Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais , Ikulu Zuhura Yunus amesema Rais Samia ameipa haki kipaumbele na ndio maana tangu aingie madarakani zaidi ya Mahabusu 2240 wameachiwa.
Zuhura ameyasema haya leo kwenye Kikao cha Wajumbe wa Tume ya Haki Jinai, DPC na Wahariri wa Vyombo vya Habari Ikulu Dar es salaam.
“Lengo la Rais Dkt. Samia ni kushughulikia malalamiko ya muda mrefu ya Wananchi kuhusu utoaji haki, tangu Rais Samia aingie madarakani zaidi ya Mahabusu 2240 wameachiwa, wakiwemo Viongozi wa Dini, Wanasiasa, Watu wengine mashuhuri na Wananchi wa kawaida ambapo waliachiwa na kurejea uraiani baada ya Rais Samia kuagiza Vyombo vya kushughuliia masuala yao, mnaweza kuona jinsi gani Mh. Rais ameipa haki kipaumbele”
“Katika hatua nyingine Mahakama za chini zimeanza kutoa hukumu na tasfiri za kiswahili ili Wananchi wafahamu vizuri mwenendo wa kesi, pia kuna Samia Legal Campaign ambayo imeanzishwa kutoa msaada wa kisheria bure, kuhusu changamoto zilizopo kwenye utoaji wa haki jinai, Rais Samia ameshaziagiza Taasisi zote za haki jinai kufanyia kazi mapendekezo ya Tume”