Ebhana kama kawaida yake Zuch Zuchero kaingia tena mtaani ambapo leo kaibuka na M-Koba maeneo ya Bonyokwa akiwa na swali tata kuhusu mambo ya usafiri barabarani hasa pale unaposafiri kwenda mkoani.
Swali la leo ni kwamba; Ikitokea mpo safarini, huku dereva akiwa katika mwendo wa haraka mathalani maeneo ya Mlima Kitonga abiria wote mkiwa kimya, ghafla unamsikia dereva analalamika akisema maisha yamemshinda bora afe, je uikiwa kama abiria utafanyaje..?