Serikali ya Malaysia imetangaza kusitisha shughuli ya kuitafuta ndege iliyopotea ya MH370 na kusema wanachukulia kama ajali ambayo iliangamiza watu wote.
Tangu kuanza kutafutwa kwa ndege hiyo iliyopotea tangu March 8 mwaka 2014 wakati ikitokea Malaysia kuelekea China hakukuwahi kuwa na dalili yoyote ya kupatikana kwa watu wala kitu chochote kilichokuwa kwenye ndege hiyo.
Maafisa wakuu wanasema shughuli ya kuitafuta ndege hiyo bado inaendelea lakini wanahisi kwamba abiria 239 waliokuwa kwenye ndege hiyo wote walifariki.
Hata hivyo Maofisa wa Serikali wa nchini hiyo walitoa taarifa leo na kusema ndugu na jamaa wa waathirika wa ndege hiyo watalipwa fidia.
Hakuna story itakayokupita mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook