Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Denis Minja (US/ZM3847) aliyemwokoa mtoto kwenye shimo la choo wilayani Ngara mkoani Kagera amevishwa cheo cha CPL (Koplo) ikiwa ni kutambua kile alichokifanya licha ya kuwa ni wajibu wake.
Zoezi la kumvisha cheo askari huyo limeambatana na gwaride rasmi na limefanyika katika ofisi za Zimamoto zilizoko bohari kuu ya mkoa katika Manispaa ya Bukoba.