Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ameagiza kuvunjwa kwa Jumuiya ya Maji Kijiji cha Berege Wilayani Mpwapwa huku akitoa onyo la ubadhilifu wa fedha za jumuiya ya watumia maji katika mradi wa maji kwenye kijiji hicho.
Ametoa kauli hiyo wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji na uendeshaji wa miradi ya maji pamoja na kuzungumza na wananchi wa kijiji hicho kilichopo halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Mkoa wa Dodoma.
Waziri Aweso alipokea malalamiko ya wananchi kuhusu jumuiya ya watumiaji maji kuwa fedha zinakusanywa lakini hazipelekwi benki.
Amebainisha kuwa jumuiya za watumia maji nchini zina changamoto kwenye usimamizi wa miradi na matumizi sahihi ya makusanyo ya fedha.