Askari mstaafu Patric Kimaro maarufu kwa jina la Sabasita mwenye umri wa miaka 61 mkazi wa Kijiji cha Mbosho, kata ya Masama Kati,Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro amesema ametumia million 13 kujijengea kaburi pamoja nakujinunulia jeneza atakalozikwa nayo siku atakayofariki
Sabasita akiongea na Ayo TV nyumbani kwake amesema jeneza hilo limetumia miezi sita hadi kukamilika na limegharimu milion tatu na wakati linaingia nyumbani kwake watu zaidi ya 100 walifika nyumbani kwake kushangaa
Amesema nyumbani kwake hamna mlinzi na hajawahi kufunga geti lake kwa zaidi ya miaka 10 na hajawahi kusikia hata kitu kimoja kikiibiwa na atakayekuja kuiba jeneza lake kuna kitu cha ziada atakachokuwa anatafuta
Miaka miwili iliyopita alianza kujichimbia kaburi hilo nakusema sababu ni ili familia isiingie gharama atakapofariki lakini atakayebadilisha nakumzika sehemu nyingine atapata matatizo