Askari wanne wa Jeshi la Polisi mkoani Arusha wamefukuzwa kazi na Maofisa wawili wa Jeshi hilo wamesimamishwa kazi kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa ya Sh100 milioni.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo ametoa taarifa hiyo leo Alhamisi Aprili 29 ,2021 na kubainisha kuwa walipokea taarifa kuhusu askari hao Aprili 19, 2021 kwamba wameomba na kupokea rushwa na uchunguzi ukaanza.
“Baada ya uchunguzi jeshi limewafukuza kazi askari wanne na kuwasimamisha kazi maofisa wawili kwa kuwa haliwezi kuvumilia tuhuma hizi,” Masejo