Mbunge wa jimbo la Kawe Askofu Josephat Gwajima akichangia mjadala wa Makadirio wa Bajeti ya Waziri Mkuu 2022/23 amesema kuna haja ya taifa kuwa mpango wa muda mrefu ili kila kiongozi anapoingia madarakani auendeleze kwa ustawi wa taifa.
“Tunahitaji Nchi yenye maono ili kila rais anayeingia madarakani afuate maono ya nhi tuliyoyaweka ipo siku kama tutaruhusu kila mtu anayeingia madarakani aongozwe na kichwa chake anavyowaza yeye kuna siku tutapata rais wa ajabu tutadondokea pua hatutaamini macho yetu” –Mbunge wa Kawe Askofu Josephat Gwajima