Hii ni good news nyingine katika soka la Tanzania, Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF September 10 limetangaza kuingia mkataba na Azam Sports wa kudhamini na kurudisha kombe la shirikisho Tanzania, mkataba huo wa kipindi cha miaka minne umesainiwa na Rais wa TFF Jamal Malinzi na mkurugenzi mtendaji mkuu wa Azam Media Rhys Torrington.
Malinzi amesaini mkataba wenye thamani ya bilioni 3.3 za kitanzania ambao utadumu katika kipindi cha miaka minne, mkataba huo wa udhamini utahusisha mdhamini kugawa vifaa kwa timu shiriki, hela ya nauli kwa timu itakayosafiri kwenda kucheza ugenini na marefa watalipwa katika viwango vile vile wanavyolipwa Ligi Kuu.
Timu zitakazoshiriki ni 64 ambazo ni mjumuisho wa timu za Ligi Kuu, Ligi daraja la kwanza na Ligi daraja la pili, timu itakayokwenda kucheza ugenini itapewa Tsh milioni 3 kama gharama ya usafiri na itakayocheza nyumbani itapewa Tsh milioni 1.
Mshindi wa kombe hilo ambalo litakuwa likiitwa Azam Sports Federation Cup (ASFC) atapata zawadi ya kombe pamoja na Tsh milioni 50 na kupewa nafasi ya kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika. Kurejea kwa kombe hili ambalo mara ya mwisho ilikuwa mwanzoni mwa miaka ya 2000, kunaondoa nafasi ya mshindi wa pili wa Ligi Kuu Tanzania bara kushiriki Kombe la shirikisho barani Afrika.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos