Siku moja baada ya Azam FC kucheza mchezo wake wa Ligi Kuu dhidi ya Ndanda FC ya Mtwara na kufanikiwa kupata ushindi wa goli 1-0, goli ambalo lilifungwa na Yahaya Mohamed dakika ya 86 ya mchezo, afisa habari wa timu hiyo Jafari Iddi ameongea na vyombo vya habari.
Baada ya mchezo Jafari Iddi ameongea kuhusiana na mipango
1- Katika mchezo dhidi ya Ndanda ulikuwa ni mchezo ambao tulitengeneza nafasi nyingi za kufunga lakini hatuwa vizuri katika umaliziaji, hilo mwalimu ameliona na analifanyia kazi ili makosa yaliyofanyika katika mchezo ule yasijirudie tena
2- Kuna wachezaji ambao walikuwa majeruhi kama mtakuwa mnakumbuka Shomari Kapombe alikwenda Afrika Kusini kufanyiwa uchunguzi, awali alikuwa ana tatizo la blood circulation baadae akatibiwa na kupata nafuu na kurudi uwanjani, lakini doctor wake anasema atakuwa anatakiwa kufanyiwa uchunguzi mara kwa mara.
3- Kuhusu kocha wetu wa kigeni yupo kwa maana ya kusubiri upatikanaji wa vibali vyake vya kufanya kazi, yupo lakini hawezi kukaa katika benchi hadi apate vibali, kama unavyofahamu wanaoomba vibali ni wengi kwa kuna kuwa na mlolongo kamilisha
VIDEO: Yanga vs Azam FC January 7 2017, Full Time 0-4